Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewashauri mawaziri na manaibu huku akiwataka kutekeleza vyema majukumu yao na kutosahau kuwa ni wabunge na uwaziri ni vyeo vya muda.

Amesema hayo leo Alhamisi Aprili mosi, 2021 baada ya kuwaapisha wabunge watatu walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambao ni mabalozi, Bashiru Ally, Liberata Mulamula na Mbarouk Nassor Mbarouk.

“Huo ndiyo uzuri wa mama, wangekuwa wenzetu wengine hapo, majeruhi wangebaki wengi lakini mama amepita katikati, kama wabunge tunamshukuru dhamana mliyoipata mtaifanyia kazi kwa imani ileile ambayo rais amewapatia.” Amesema Spika Ndugai

“Nyinyi ni wabunge kama sisi hilo ndiyo la msingi yaani hapa bungeni ndiyo nyumbani, huko mmekwenda matembezi tu likitokea jambo la kutokea mnarudi hapa kwa hiyo tusijisahau sana jamani msisahau kuwa ushauri wa wabunge ni muhimu sana kwa sababu ni ushauri wa wananchi,” amesema Spika Ndugai.

AS Vita Club kutua Dar leo
Dkt. Bashiru na wenzake wala kiapo Bungeni