Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia sasa China imewekeza zaidi ya dola bilioni 10 katika maeneo mbalimbali nchini na ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wengine zaidi, ambapo takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania – TIC, zinaonesha kuna zaidi ya miradi 1,134 iliyosajiliwa kutoka kwa Makampuni ya China.

Mjaliwa ameyasema hayo jioni ya Septemba 25, 2023, wakati akifunga Kongamano la Uwekezaji na Biashara baina ya Tanzania na China, kwa udhamini wa Jimbo la Zhejiang (Jinhua) jijini Dar es Salaam na kwamba uwepo wa makampuni hayo umechangia ajira kwa Watanzania.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema, “miaka 10 iliyopita, China ilikuwa nchi ya sita miongoni wa wawekezaji wakubwa hapa nchini ikitanguliwa na Uingereza, Marekani, Afrika Kusini na Kenya. Lakini kutokana uwekezaji wa sasa, imekuwa nchi ya kwanza kwa uwekezaji hapa nchini.”

Aidha, ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira bora na rafiki ya uwekezaji ikiwemo kufanya maboresho ya sera ya uwekezaji na imefanya maboresho kwa kuondoa urasimu, mlolongo wa vikwazo kwa kuweka one stop centre kwenye kituo cha uwekezaji, huku akitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekeze Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi hasa kwenye maeneo ya ujenzi wa makazi na ofisi..

Masauni ataka ushirikiano utekelezaji Sera Polisi Jamii
Mabadiliko: Rais Samia aivunja REA, Maharage ahamishwa tena