Umoja wa Wanawake Tanzania – UWT, umesikitishwa na kitendo cha Baraza la Wanawake la Chadema – BAWACHA, kutoheshimu mamlaka na kutumia lugha ya kejeli dhidi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Marry Chatanda na kusema katika maandamano hayo ya Mei 11, 2023 CHADEMA walibeba mabango na kutoa kauli zisizo za kiuungwana zilizo muhusisha moja kwa moja Rais Samia.
Amesema, umoja huo hautovumilia kauli hizo na utasimama kudumisha misingi ya kuheshimiana hasa wakati huu ambapo Rais Dkt. Samia amekuwa mstari wa mbele kujenga demokrasia imara na utawala wa sheria.
“UWT haitokuwa tayari kuvumilia uhuru huo kutumika vibaya mfano lugha ya matusi, udhalilishaji na wenye kutweza utu na hasa ukiwa unamlenga Rais Dk. Samia na mkuu wa muhimili wa Bunge, Spika Dk. Tulia Ackson,” amesisitiza Chatanda.