Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC kwa kushirikiana na Mzabuni wa Ubunifu na Uuzaji wa jezi za klabu hiyo, umeamua kuziachia jezi mpya za msimu 2021/22, leo Ijumaa Septemba 03.

Simba SC na Mzambuni (Kampuni Vunja Bei) walitangaza Jumamosi (Septemba 04) kuwa siku ramsi ya uzinduzi wa jezi za klabu hiyo na kuanza kuzuiza siku hiyo.

Kaimu Afisa Habari wa Simba SC Ezekiel Kamwaga amezungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam, na kusema uhitaji wa jezi za klabu ya Simba kutoka kwa Mashabiki na Wanachama umewafanya kuziachia siku moja kabla.

“Maombi ya jezi kutoka kwa mashabiki wa Simba yamekuwa makubwa sana na uongozi umeona ni vyema kuwasikiliza. Natangaza rasmi kwamba kuanzia sasa jezi mpya za Simba zinapatikana sasa kwenye maduka ya Vunja Bei nchi nzima” amesema Ezekiel Kamwaga.

Kuhusu taarifa za kuvuja kwa Jezi za Simba SC, na kuepelekea maamuzi ya kutangaa kuziachia kabla ya tarehe rasmi ya uzinduzi iliyokua imetangaza awali, Kamwaga amesema hawezi kuthibitisha suala hilo, japo amekiri katika ulimwengu wa sasa suala hilo linawezekana.

Hata hivyo Kamwaga amekemea tabia ya baadhi ya watu waliothubutu kufanya njama chafu za kuvujisha jezi, kwa kusema wanatengeneza uhasama ambao hautalisaidia soka la Tanzania ambalo limeanza kupiga hatua kimataifa.

“Kuna timu kama Coastal Union wametoa jezi lakini hazikuvuja, imefika Simba jezi imevuja. Hii ni Tabia mbaya. Kwa nini uvujishe jezi ya Timu? Tukianza ‘utani wa jadi’ wa kuvujishana jezi, Tunapokwenda itakuwa ni vita.” amesema Kamwaga.

Hata hivyo Uongozi wa Simba SC, umesisitiza shughuli za kutambulisha jezi mpya, katika hafla maalum itakayofanyika jijini Dar es salaam.

Rais Mwinyi akagua mradi jengo la mama na mtoto hospitali ya chakechake
Kim Poulsen: Wamepambana sana