Abel Paul, Jeshi la Polisi – Dar es Salaam.

Askari wa Jeshi Polisi nchini, wameitumia vyema nafasi ya kufanya jitihada katika masuala ya Polisi jamii, ili kutokomeza uhalifu baada ya Askari Polisi kutoka nchini Ujeruman na Thailand kutoa uzoefu wao katika masuala ya Polisi Jamii na namna wanavyowahudumia raia.

Akiongea mara baada ya mafunzo hayo Profesa Krisanaphong Poothakool, kutoka Thailand amesema Polisi awezi kufanya kazi mwenyewe bila kushirikisha jamii ambapo amebainisha kuwa Polisi akiamiwa na jamii ananafasi kubwa ya kupata taarifa.

Awali, kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Urich Matei ambaye amemwakilisha Kamishna wa kamisheni ya ushirikishwaji Jamii, CP Faustine Shilogile amesema dira ya Polisi kwa sasa chini ya Mkuu wa Jeshi ni kushirikisha jamii katika kukabiliana na uhalifu Katika jamii ambapo ameongeza kuwa watumishi wa serkali za mitaa kushirikiana na askari kata.

Amewataka maofisa wanafunzi waliopata elimu hiyo na uzoefu kutoka kwa Polisi wa Thailand na Ujerumani kutumiwa vyema elimu waliyo ipata Kwenda kutoa huduma bora Zaidi kwa wananchi wanao litegemea Jeshi la Polisi.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Hanns Seideil Foundation, Karl-Peter Schönfisch amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camillus Wambura kwa matokeo chanya wa mfumo wa Polisi jamii kwani wamejifunza namna wanavyoshirikisha jamii kutatua uhalifu.

Naye Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Dkt. Lazaro Mambosasa amewashukuru askari hao kwa kubadilisha uzoefu licha ya kuwa wao wako mbele kiteknolojia katika kukabiliana na uhalifu ambapo amebainisha kuwa wamejifunza vitu vingi ambavyo vtakuwa na faida kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Nacho Fernandez asaini mmoja Real Madrid
Azam FC yamkana Bernard Morrison