Kocha wa Manchester United Louis van Gaal ana amini kuwa timu hiyo inaweza kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuonyesha kandanda safi wakati wakicheza na Liverpool na kuibuka na ushindi mwembamba wa goli moja kwa bila hapo jana.

Goli la Man United lilifungwa na Wayne Rooney dakika ya 78 na kuandika historia ya kuifunga liverpool wakiwa Anfield kwa mara ya kwanza tangu 2005.

Akiongea baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana, amesema kuwa malengo yake ni kumaliza akiwa na ubingwa katika msimu huu licha ya kuwa wapo nyuma kwa pointi kadhaa.

“Kuifunga Liverpool ilikuwa muhimu sana na ukizingatia washindani wetu walipoteza pointi  na ukiangalia uwiano wa pointi wa anayeongoza ligi tunaweza kuwashinda na kuwapindua,” Alisema Van Gaal

Ufisadi wa Miss Tanzania wapelekea Serikali Kuishushia rungu zito benki ya Stanbic
FC Bayern Munich Watupa Jicho Hispania

Comments

comments