Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa hababaishwi na hamu ya Pep Guardiola kuifunza kilabu hiyo.

Kocha huyo wa Bayern Munich ametangaza kwamba aitaihama kilabu hiyo mwezi Mei baada ya kuifunza kwa misimu mitatu.

Mkufunzi huyo wa zamani wa Barcelona ameshirikishwa na kilabu zote mbili za Manchester pamoja na Chelsea na Arsenal.

”Ana hamu na anataka kuujua utamaaduni wa Uingereza na ligi yao kuu.Ni vizuri kwamba anataka kufanya hivyo”,alisema Van Gaal.

Naelekea kilele cha kazi yangu kwa hivyo kwangu mimi sio kitu cha kunivutia.Kitu muhimu ni vile nitakavyoifunza Manchester United wakati huu wa kanadarasi yangu”,alimaliza Van Gaal.

Van Gaal mwenye umri wa miaka 64 yuko na kandarasi na kilabu hiyo hadi mwisho wa msimu ujao lakini kazi yake imekosolewa baada ya kucheza mechi nane bila ushindi katika ligi msururu ulioisha wikendi iliopita baada ya kuishinda Swansea 2-1.

 

Bulembo: Lowassa alitutikisa CCM
Picha: Mchepuko Mpya wa Tyga kutoka Brazil unaomliza Kylie

Comments

comments