Meneja wa klabu ya Man Utd, Louis van Gaal amesema anapata wakati mgumu dhidi ya familia yake ambayo imekua ikimshinikiza aachane na masuala ya soka.

Van Gaal amesema familia yake imekua ikionyesha kumuhitaji katika kipindi hiki na wakati mwingine mkewe huenda mbali zaidi kwa kumtaka aachane na masuala ya mpira wa miguu kwa kutangaza kustaafu.

Meneja huyo kutoka nchini Uholanzi amesema inamuuwia vigumu kufanya maamuzi hayo, kutokana na mkataba alionao kwa sasa ndani ya klabu ya Man Utd ambao ataendelea kuutumikia hadi mwaka 2017.

Amesema mara kadhaa amekua akimtaka mkewe kuwa na subra kwa kumuaminisha muda wa miezi 18 iliyosalia kwenye mkataba wake sio mrefu, hivyo anapaswa kuheshimu na kuamini ipo siku atatulia nyumbani na familia.

Van Gaal aliianza kujishughulisha na soka 1972 akiwa mchezaji wa klabu ya PSV ya nchini kwao Uholanzi na alitangaza kustaafu mwaka 1987 akiwa na klabu ya AZ Alkamar na baada ya hapo alijiingiza kwenye ukocha kuanzia mwaka 1988 na mpaka sasa yupo katika tasnia hiyo.

‘Toroka Uje Ya Ukawa’ Kusomba Vigogo Hawa Wa CCM..?
‘Ukawa Wana Uhakika Wa Kushindwa, Wameshakata Tamaa’