Klabu ya Manchester United imemuorodhesha kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes katika kikosi chake cha wachezaji 25 watakaocheza Ligi Kuu ya England.

Valdes ametengwa na kocha Louis Van Gaal baada ya mwalimu huyo kudai kwamba mlinda mlango huyo aligoma kuchezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 jambo ambalo lilimfanya atemwe kwenye ziara ya kujiandaa na msimu nchini Marekani.

Tangu hapo, kipa huyo mwenye umri wa miaka 33 amekuwa akifanya mazoezi kivyake na alitarajiwa kusaini Besiktas mwishoni mwa wiki, lakini akiwa hoteli ya Uwanja wa Ndege wa Manchester tayari kwa safari ya kwenda kukamilisha uhamisho wake, dili likabuma na dirisha likafungwa.

Kikosi kamili kilichowasilishwa FA ni Daley Blind, Michael Carrick, Matteo Darmian, Matteo, David de Gea, Marouane Fellaini, Ander Herrera, Sam Johnstone, Phil Jones, Will Keane, Jesse Lingard na  Juan Mata

Wengine ni Marcos Rojo, Sergio Romero, Wayne Rooney, Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger, Chris Smalling, Victor Valdes, Antonio Valencia, Guillermo Varela na Ashley Young.

Spurs Yamtema Kiaina Emmanuel Adebayor
Dk. Slaa Ajibu Alikotoa Fedha Za Kugharamia Mkutano Wake Na Matangazo