Ushindi wa mabao matatu kwa sifuri uliowapa Arsenal point tatu nyumbani, umeshindwa kumpa nafasi meneja wa klabu ya Man Utd, Louis van Gaal kuzungumza kwa busara mbele ya vyombo vya habari na badala yake alijikuta akibwatuka.

Van Gaal, alionyesha hasira za kupoteza mchezo wa jana jioni kwa kusema kikosi chake kilikua dhaifu na mpaka alishindwa kukipachika jina la kushindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa namna ya kufanya hivyo.

Van Gaal alisema haikuwa matarajio yake kuona wachezaji wa Man Utd wakicheza hovyo na kuruhusu mabao matatu ndani ya dakika 20 za kipindi cha kwanza, hali ambayo anaiona kama anguko kubwa katika mipango aliyokua amedhamiria itumike kwenye mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Emirates.

Alisema ilikua ni vigumu kwao kuondoka na point tatu kwenye uwanja wa ugenini kutokana na kuanza vibaya mchezo huo, hali ambayo iliwapa nafasi Arsenal kutakata na kujipatia mabao ya haraka ambayo yalidumu hadi dakika 90 zilipokamilika.

Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Uholanzi aliahidi kulitafutia ufumbuzi tatizo lililojitokeza jana jioni kwa kuutumia muda wa juma moja na nusu ambapo wachezaji watakua na timu zao za taifa na watakaporejea shughuli ya kurekebisha makossa itaanza rasmi.

Lakini pamoja na kulalamika huko, Van Gaal amewapongeza Arsenal kwa kusisitiza walicheza vizuri na walizitumia vyema nafasi walizozipata.

Kufungwa katika mchezo wa jana, kumeifanya Man Utd kuporomoka kwa nafasi moja kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa huku wakiwa sawa na Arsenal katika upande wa point.

Zlatan Ibrahimovic Amchakaza Pauleta
Liverpool Yawawinda Klopp, Ancelotti