Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Ruud van Nistelrooy amesema Romelu Lukaku ana sifa ya kuwa mchezaji mkubwa na muhimu Old Trafford baada ya mchezaji huyo wa Ubelgiji kuwa na mwanzo mzuri akiwa amefunga mabao sita mpaka sasa  msimu huu.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alisajiliwa na Jose Mourinho kutoka Everton kwa makataba wa miaka mitano  amefunga mabao 6 katika michezo sita aliyoichezea Man Utd.
Van Nistelrooy aliyeifungia Man Utd mabao 150 katiaka michezo 219 anaamini Lukaku anaweza kufikia idadi ya mabao aliyofunga pamoja na mzigo mkubwa wa majukumu aliyonayo Man Utd.
”Lukaku amekuwa na mwazo mzuri pamoja na presha iliyopo juu yake kama msambuliaji wa Manchester aliyenunuliwa kwa kiasi kikubwa cha pesa” alisema Van Nistelrooy.

Van Nistelrooy aliifungia Man Utd mabao 150 katika michezo 219

Leo Lukaku atacheza kwa mara yan kwanza dhidi ya timu yake ya zamani ya Everton wakati timu hiyo itakapoikabili Man Utd katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa katika dimba la Old Trafford.

Dkt. Shein kuongoza Kikao cha Kamati Kuu CCM
Bulyanhulu kukwepa zigo la makinikia