Tetesi za usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi, Robin van Persie kuelekea klabu ya Fenerbahce ya Uturuki zinaendelea kushika kasi ambapo kwa sasa imeelezwa kuwa mambo yamekaa vizuri.

Kituo cha televisheni cha Sky cha Uingereza, kimeripoti kwamba uongozi wa klabu ya Fenerbahce umefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa mkataba wa miaka minne.

Mkurugenzi wa klabu ya Fenerbahce, Guiliano Terraneo ameripotiwa kuwa jijini London kwa mazungumzo ya kina ya uhamisho wa Robin van Persie, ambaye mkataba wake wa kuitumikia Man Utd umesaliwa na mwaka mmoja.

Mazungumzo kati ya kiongozi huyo klabu ya Fenerbahce, yameelezawa kudumu kwa siku kadhaa, na matokeo chanya yameonekana kutokana na mikakati inayoendelea baina ya pande hizo mbili.

Kituo hicho cha televisheni kimeeleza kwamba, huenda mwishoni mwa juma hili, Van Persie akatangazwa kuwa mchezaji rasmi wa klabu ya Fenerbahce, baada ya kumaliza taratibu za uhamisho wake likiwemo suala la kupimwa afya.

Sterling Aeleza Sababu Ya Kutohudhuria Mazoezi Ya Liverpool
Hummels: Bado Nipo-Nipo Sana BVB