Siku chache baada ya mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi, Robin van Persie, kuhamishia maisha yake nchini Uturuki kwenye klabu ya Fenerbahce, mambo yanaonekana kuwa shwari kwenye familia ya mchezaji huyo.

Van Parsie ambaye alikuwa akiitumikia Man Utd kabla ya kufungasha virago na kuelekea Ulaya ya Mashariki, amemvuta mwanae Shaqueel na kumuidhinisha kimkataba kwenye kituo cha kulea na kuendeleza vipaji cha klabu ya Fenerbahce.

Uongozi wa Fenerbahce umethibitisha kukamilishwa kwa dili hilo huku ukiamini wamepata mrithi wa mshambuliaji huyo katika maisha ya baadae ya klabu hiyo iliyomaliza kwenye nafasi ya pili msimu uliopita.

Mbali na Shaqueel kujiunga na kituo cha vijana klabuni hapo, pia mtoto wa kike wa Van Parsie amejiunga na kituo cha kulea na kuendeleza vijapi vya mchezo wa sarakati kinachomilikiwa na Fenerbahce.

Aliyebaguliwa Ufaransa Achachamaa
Josep Bartomeu: Vyombo Vya Habari Acheni Uzushi