Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema wachezaji wake walipambana vilivyo dhidi ya Plateau United ili kusaka matokeo kwenye uwanja wa nyumbani, lakini haikuwa bahati kwao na ana imani hatua inayokuja watakutana na timu ngumu katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Sven alisema ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata ugenini ulikuwa mtaji mzuri kwao kwa kuwavusha na kucheza katika hatua ya kwanza, hivyo sasa wanajipanga kwa mechi ijayo ambayo anaamini itakuwa ngumu zaidi.

“Tulicheza vizuri hata wapinzani wetu walijipanga kutafuta ushindi, lakini bao la ugenini kwetu limetufaidisha na sasa tunaenda kujipanga dhidi ya wapinzani wetu katika hatua nyingine ambayo ni timu nzuri zaidi ya hii tuliyocheza nayo.

“Tunaenda kujipanga na kufanyia kazi upungufu wetu wa mechi zilizopita dhidi ya Plateau, tunatakiwa kuwa makini katika hatua inayofuata kuhakikisha tunafikia malengo yetu ya kucheza hatua ya nusu fainali,” alisema Sven.

Simba SC itaanzia ugenini katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe kati ya Desemba 22-23 kabla ya kurudiana kati ya Januari Januari 5-6 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 8, 2020
Wengine wawili waula uwakilishi Zanzibar