Vanessa Mdee ameamua kukifungukia kituo cha runinga cha Trace Mziki kwa kile alichokieleza kuwa kimekuwa na tabia ya upendeleo kwa muda mrefu.
Mwimbaji huyo ambaye mwaka huu anashikilia rekodi nzito ya Albam yake ‘Money Mondays’ kushika nafasi ya kwanza Afrika Mashariki kwa mauzo mtandaoni, ametumia Twitter kushusha pumzi ya dukuduku lake dhidi ya TraceMziki.
“Wacha niseme tu @TraceMziki imekuwa station fulani ya upendeleo kwa wasani kadhaaa kwa muda mrefu sana. Kuna ule upendeleo wa kuficha alafu kuna ile LIVE BILA CHENGA,” ameandika kwenye Tweet ya kwanza.
Wacha niseme tu @TraceMziki imekuwa station fulani ya upendeleo kwa wasani kadhaaa kwa muda mrefu sana. Kuna ule upendeleo wa kuficha alafu kuna ile LIVE BILA CHENGA.
— VeeMoney #MoneyMondays (@VanessaMdee) December 13, 2018
“Na haikuwa hivyo mwanzoni, sasa nauliza @TraceMziki tunakwama wapi?” ameongeza kwenye tweet nyingine.
Malalamiko ya Vee Money thidi ya Trace Music yalimuibua pia Bill Nas ambaye amejibu akiunga mkono, “Mimi ndo Sikumbuki Lini Mara Ya Mwisho nimechezwa Huko !!!”
Hata hivyo, malalamiko ya mwimbaji huyo wa ‘Bambino’ hakuelezea upendeleo huo ni wa namna gani, hali iliyomuibua mchangiaji mmoja anayejiita Mike Fleva Omwony kumuuliza maswali manne.
Katika maswali yake kwa Vanessa, Mike aliuliza akitaka kupata taarifa zaidi kuhusu upendeleo huo 1. Hawapigi nyimbo zako? 2. Wanacheza kupilitiza nyimbo za nchi moja? 3. Msanii mmoja ambaye haumkubali anachezwa sana? 4. Vyote kwa pamoja?
Vee Money ambaye hivi karibuni ameachia ‘Bambino’ aliyomshirikisha Reekado Banks wa Nigeria, hakutoa ufafanuzi kuhusu hilo.