Vanessa Mdee anazidi kupanda ngazi za kimataifa na huenda mwaka huu ukawa mwaka wake mkubwa zaidi utakaomuweka katika ngazi nyingine.

Mkali huyo wa ‘Kisela’ ametajwa kushindania vipengele vitatu katika tuzo tano kubwa za Kimataifa.

Tuzo hizo ni pamoja na AFRIMA (Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki), Nigeria Entertainment Awards (Msanii Bora wa Afrika), Africa Entertainment Awards USA (Wimbo Bora wa Msanii wa Kike), African Entertainment Awards (Msanii Bora wa Kike wa Kimataifa).

Vee Money amepata nafasi hizo kutokana na kazi zake nzuri ambazo amekuwa akizifanya na kwa miaka miwili mfululizo ameachia ‘collabo’ za kimataifa ikiwa ni pamoja na Mr. P wa P-Square, K.O wa Afrika Kusini na wengine.

Mbali na kuwashirikisha, naye ameshirikishwa na wasanii wengi wa kimataifa wakiwemo Orezi wa Nigeria na Tay Grin wa Malawi.

Kumuwezesha Vanessa kunyakua tuzo hizo na kuiweka Tanzania kwenye ramani ya juu zaidi hasa kwa wasanii wa kike, bofya link zifuatazo umpigie kura:

AFRIMA(best female eastern Africa)?

https://www.afrima.org/AFRIMAVOTING/home?mcat=Regional%20Category&scat=Best%20Female%20in%20Eastern%20Africa

AFRIMMA(best female east Africa)

http://afrimma.com/afirimma-2017-nomination-polls/

NEAAWARDS(African female artist)

https://www.neaawards.org/africa-non-nigerian-best-actor

AEAUSA(best female single)

http://www.aeausa.net/

AEAWARDS (best International female Artist)

http://aeawards.ca/nominees.html

Pogba marufuku kucheza mpira wa kikapu
Barcelona kuikabili Atletico Madrid bila mashabiki