Vanessa Mdee amevunja ukimya baada ya kushambuliwa mara kadhaa kwenye Instagram kwa madai kuwa hakuhudhuria misiba ya hivi karibuni ya watu wake wa karibu katika tasnina, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, mtangazaji nguli, Ephraim Kibonde na rapa Godzilla.

Vanessa ambaye amewahi kuwa mfanyakazi wa Clouds Media Group, ametumia Instagram kuwajibu watu waliomhukumu kwa kutoona picha yoyote aliyopost akiwa msibani, akieleza kuwa alikuwepo lakini hataki kupost picha kudhihirisha kwa sababu maalum.

Vee Money ambaye alikuwa akiweka picha zao tu na kuwatakia mapumziko mema ya milele lakini hakuweka picha inayomuonesha akihudhuria kuwazika au kuwaaga, alikumbusha machungu ya misiba inayomtesa moyoni, ikiwa ni pamoja na msiba wa baba yake mzazi pamoja na dada yake. Anaamini sio lazima kuweka mitandaoni jinsi ulivyohudhuria msiba.

“Niliona nipotezee lakini naomba niseme once and for all. Misiba na mazishi ni kama ibada, ukishiriki sio habari ya kutangaza kama tamasha. Nimeona watu wanataka kunishikilia bango kama mtu asiyehudhuria au asiyeshiriki katika ibada hizi. Kama unataka kufaham nilikuwepo katika misiba yote ya hivi karibuni lakini sikupenda kutangaza uwepo wangu kutokana na kupitia misiba mizito katika maisha yangu kama watu wengine wengi. Siku ya kesho itakuwa miaka 12 tangu nimpoteze baba yangu mzazi na mwaka huu ni miaka miwili tangu nimpoteze Dada yangu ( mtoto wa kwanza wa baba) i bet you didn’t even know, why? Because I prefer to silently pray for the family and loved ones, I’ve found that only God can bring some relief in these situations. Mtu akifiwa anapitia mambo mengi na anahitaji faraja. Nadhani nimeeleweka. Asanteni na Mungu awatunze wote na familia zenu.”

 

View this post on Instagram

 

Niliona nipotezee lakini naomba niseme once and for all. Misiba na mazishi ni kama ibada, ukishiriki sio habari ya kutangaza kama tamasha. Nimeona watu wanataka kunishikilia bango kama mtu asiyehudhuria au asiyeshiriki katika ibada hizi. Kama unataka kufaham nilikuwepo katika misiba yote ya hivi karibuni lakini sikupenda kutangaza uwepo wangu kutokana na kupitia misiba mizito katika maisha yangu kama watu wengine wengi. Siku ya kesho itakuwa miaka 12 tangu nimpoteze baba yangu mzazi na mwaka huu ni miaka miwili tangu nimpoteze Dada yangu ( mtoto wa kwanza wa baba) i bet you didn’t even know, why? Because I prefer to silently pray for the family and loved ones, I’ve found that only God can bring some relief in these situations. Mtu akifiwa anapitia mambo mengi na anahitaji faraja. Nadhani nimeeleweka. Asanteni na Mungu awatunze wote na familia zenu.

A post shared by VeeMoney ?? (@vanessamdee) on


Ujumbe huu uliungwa mkono na watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ben Pol na Cynthia Masasi Mziray ambaye mdau kwenye kiwanda cha burudani na mwanzilishi wa ‘The Trendy Show’ ambaye alikueleza jinsi alivyokutana na Vanessa na mpenzi wake Jux kwenye msiba wa Ruge.

Cynthia anaamini wakati mwingine msiba unapokuwa mzito kwako, kuweka picha mtandaoni linakuwa suala la mwisho kabisa.

“Well said mdogo wangu @vanessamdee hakuna kitu kinauma kama msiba especially if you personally know the person who died… personally namjua marehemu Ruge kama kaka/mshauri wangu mkubwa sana na marehemu Ephraim tulikuwa wote msibani kwa Ruge tumepiga story mud mrefuu sana na RC Makonda na hakuna picha tuliyopiga… Yani eti mtu anaenda msibani anapiga picha na kila mtu halafu anapest kabisa (I’m sure angekuwa kafiwa yeye wala hizo nguvu asingepata za kupiga picha) it’s very sad kwakweli.. Mimi binafsi nimeenda misiba yote miwili na picha hata moja sijapiga.. I know how it hurts to lose a person that you love so taking a pich is the last thing I would do… Nimekuona msibani na hata wakati wa kuondoka tumeondoka na Jux na Ice cream tukala hapo barabarani but just because hamkupost mmepiga picha people will always talk the talk… Nimekupenda saana kwa hilo ni funzo kwa watu. Misiba sio shemu ya kwenda kushow off na mapicha picha ili iweje? May their soul rest in paradise.”

Polepole ‘alivyomfagilia’ Lowassa
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 10, 2019