Nyota ya kukubalika kwa kazi na uzuri alionao Vanessa Mdee ndani na nje ya Tanzania iliwahi kumgusa Jay Z aka Hov mwenye uwezo mkubwa wa ku-detect sura za biashara walipokutana jijini Lagos, Nigeria.

Mwimbaji huyo mrembo, mzawa wa Arusha aliyewahi kupata nafasi ya kung’aa na kushinda nafasi ya kuwa mtangazaji wa MTV, amekiambia kipindi cha Chill na Sky kinachotayarishwa na mhariri mkuu wa Bongo 5, Fredrick Bundala aka Skywalker kuwa aliwahi kukutana na Jay Z na mapokeo yake yalikuwa mazuri tofauti na wengi wanavyomfikiria.

Vee Money ambaye sasa anawania tuzo za MTV/MAMA 2015 katika kipengele cha msanii bora wa kike Afrika ameeeleza kuwa alikutana na rapa huyo katika tuzo za MTV zilizofanyika jijini hapo ambapo yeye alikuwa na jukumu la kuwahoji wasanii maarufu waliopita kwenye red carpet huku ikiwa ni siku yak e ya kwanza kufanya kazi hiyo.

“[niliwahi kukutana na Jay Z] Yes, ooh my God! I was so nervous, lakini bahati nzuri nilikuwa sim-interview. Halafu mimi nina ugonjwa fulani hivi, kama nampenda mtu au nam-admire mtu nanayamazaga kimyaa,” alisema Vanessa.

“I was just like…. And he was so nice, he was like ‘ooh my God you’re so pretty’, like ‘they had to put your face on MTV’. I was like ooh my God ataniua…sasa sijui hata jinsi ya kujibu ni kama lugha inanipotea,” Vee Money alisimulia.

Vanessa aliendelea kueleza kuwa Hov sio mtu wa maringo kama watu wanavyomchukulia, huenda anaonekana hivyo katika sura ya biashara lakini akiwa nje ya jicho la media ni mtu poa sana.

“He was so nice, very calm. Nikamkumbusha kwamba walikuja Tanzania… and he was like ‘yeah Tanzania is a beautiful country’. Yaani very nice guy, very diplomatic. Halafu hana majidai ya ajabu, labda kwa sababu mimi nilikuwa back stage and there was nobody in backstage,” alieleza Vee Money.

Mbali na Jay Z, Vanessa anasema aliongea na Kanye West pia na kipindi hicho alikuwa ameanza uhusiano na Kim Kardashian kimyakimya kwa hiyo walikuwa naye. Anasema Kanye alimuonesha hadi kabati lake la nguo.

Alichokiona Jay Z kuwa Vanessa ni sura ya biashara kimeendelea kuonekana ambapo hivi karibuni mrembo huyo amekuwa kisura wa bidhaa mbalimbali kubwa nchini.

Vanessa ambaye ni mshindi wa tuzo za KTMA kwa miaka miwili mfululizo, anaendelea kufanya vizuri kwenye muziki pia ambapo wimbo wake wa ‘Nobody But Me’ aliomshirikisha K.O inafanya vizuri kwenye media za ndani na media za kimataifa.

Yanga Yakubali Kuwaachia Wachezaji Watatu
Iggy Azalea adai Media Zinamkosanisha na Britney Spears