Mwananmuziki maarufu wa bongo fleva anayeishi Marekani kwa sasa Vanessa Mdee, amekanusha taarifa za mitandaoni ambazo zinadai kwamba amejifungua mtoto na mpenzi wake Rotimi hali ambayo imempanikisha mama yake aliyepo Jijini Arusha.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vanessa Mdee ametumia Insta Story yake baada ya kushea video clip iliyokuwa na ujumbe wa kukanusha taarifa hizo kwa kusema.
“Sina mtoto ‘you freak my mom out’ mama wa watu yupo zake Arusha mnaanza kumpanikisha kwamba nimezaa, aliyewaambia nimezaa ni nani”.amesema Vanessa
Mpka sasa ni takribani miaka miwili tangu Vanessa Mdee na Rotimi waanze mahusiano yao na tayari wameshachumbiana lakini mashabiki wao wamekuwa wakitamani couple hiyo ipate mtoto.