Mwanamuziki wa bongo fleva aliyetangaza kuacha muziki Vanessa Mdee, amevalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Rotimi ambaye ni msanii wa filamu na mwanamuziki nchi Marekani ambao wanaishi wote kwa sasa nchini chini humo.

Kupitia ‘videos clip’ ambazo zimepostiwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha Rotimi akiwa amepiga magoti mbele ya Vanessa Mdee huku akimvalisha pete hiyo ya uchumba.

”Mwaka mmoja na nusu uliopita ulimwengu ulinicheka niliposema kuwa wewe ulikuwa mume wangu siku chache tuu baada ya kukutana na wewe, Sikuwalaumu, baada ya yote ni hisia isiyo ya kawaida na isiyoeleweka wakati unakutana na roho yako”.ameandika Vanessa

Ikumbukwe tu mwanzoni mwa mwezi wa kumi mwaka 2020, Vanessa Mdee na Rotimi walishea picha mitandaoni zikiwaonyesha wamechora ‘tattoo’ zenye majina yao kwenye miili yao.

Penzi la wawili hao lilianza Oktoba 2019, baada ya Vanessa Mdee kuachana na mkali wa RnB Bongo Juma Jux ambao walidumu kwa miaka 6.

Mwigulu: Ufanyike utafiti wa wapiga kura
Serikali yasitisha makongamano, mikutano ya mkesha wa mwaka mpya