Urembo, uzuri, kipaji na hali ya kifedha alivyonavyo Vanessa Mdee kinaweza kuwa chanzo kikubwa cha kuamini kuwa sasa anaweza kuwa tayari kufunga pingu za maisha na kijana wa Kitanzania kwa kuwa ameshapata vingi vya maisha pia. Na of course’ kwa sasa ukisikia tangazo la ndoa ya Vee Money utajua kwa haraka haraka ‘Jux’ kavuta jiko!

Hata hivyo, akiongea na Morning Trumpet ya Azam TV mapema leo, mrembo huyo, msomi na mwenye vipaji vingi ameweka wazi kuwa hajapata wazo na hajawa tayari kuingia kwenye ndoa hivi karibuni.

Vanessa ambaye hivi karibuni ameachia video ya wimbo mpya ‘Niroge’, amesema kuwa hana wazo la ndoa kwa kuwa hivi sasa amejikita zaidi katika muziki wake ili aweze kupiga hatua zaidi kimataifa hivyo saula la ndoa halijapata nafasi akilini mwake.

'Bei za rushwa kwa wabunge zinajulikana'
Makonda kuwakamata watakampa taarifa kuhusu Rushwa makanisani