Malkia wa Bongo Fleva anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi, Vanessa Mdee ameweka wazi juu ya mkataba mpya alioingia na kampuni kubwa duniani ya usambazaji wa muziki inayojulikana kama Universal Music Group, mwishoni mwa mwaka huu.

Universal Music Group ni kampuni kubwa ya muziki duniani ikiwa imesajili wanamuziki wakubwa na wanaofanya vizuri kutoka Marekani.

Kmaouni hiyo imejikita zaidi katika kuandaa miziki, kuandika nyimbo mbalimbali, kurekodi, kusambaza na kutangaza kazi za wanamuziki waliosajiliwa chini ya kampuni hiyo duniani kote kwa kutumia teknolojia mpya.

Wanamuziki wakubwa waliopo chini ya kampuni hiyo ni kama Kanye West, Lady Gaga, Selena Gomez, Mariah Carey, Adele, Enrique Iglesias, Lily wayne, Taylor Swift, Jay Z, Chriss Cornell, Maroon 5, Will Smith, na wengine wengi amabao ni wasanii wakubwa nchini Marekani.

Hivyo Vee Money kupitia ukurasa wake wa instagram amewaambia mashabiki juu ya usajili wake katika kampuni hiyo kubwa ya muziki duniani.

“Nimeona niitumie siku na fursa hii kuwajulisha wapendwa mashabiki zangu mwanzoni mwa mwaka huu. Nilipitia changamoto nyingi Sana. Lakini kwa neema za Mungu. Nilitoka mahali pale na sio kuona baraka tu bali na maajabu mengi yaliyotokea kwenye maisha yangu ikiwemo kuwa mmoja wa familia ya Universal Music Group in a unique joint signing between Universal Music Germany, Airforce1 na Universal Music Group” Vanessa Mdee.

Ameongeza “hii ni mara ya kwanza kwa msanii wa kiafrika kupata deal ya aina hii yenye mkwanja mrefuu sana…Hii ni habari njema kwa mashabiki wangu na ndiyo kwanza tumeanza. Mambo makubwa zaidi yanakuja. Kumbuka kila mwisho wa Jumapili ndiyo mwanzo wa Jumatatu, usiogope kuanza upya” Vanessa Mdee,.

Vanessa amewashukuru mashabiki zake, ndugu jamaa na marafiki ambao walikuwa pamoja na yeye kuanzia mwaka kuanza japo ulikuwa na changamoto mpaka sasa anbapo mwaka unaelekea kuisha.

 

 

 

Trump atangaza mkakati mpya wa kiusalama
Ikosoeni serikali kwa utaratibu- JPM