Mchezaji nyota wa tenisi kutoka Uingereza Johanna Konta amemshinda Venus Williams, kwa seti mbili kwa sifuri ambazo ni 6-4 6-2 na kufika raundi ya pili katika michuano ya Australian Open mjini Melbourne, nchini Australia.

Konta, mwenye umri wa miaka 24, alipata ushindi kwa kutumia dakika 79 huku bingwa wa Grand Slam, Venus Williams, ambaye alikuwa amefunga bendeji katika paja lake la kushoto, akionekana kutatizika.

“Droo ilipofanywa na nikaona nilikuwa nimepangwa kucheza na nani, niliomba tu niweze kudumu uwanjani zadi ya saa moja,” amesema Konta.

Konta, aliyefika hatua ya 16 bora katika US Open mwaka 2015, sasa atakutana na mshindi kati ya Carina Witthoeft na Saisai Zheng, katika raundi ya pili.

Konta anaeshika nafasi ya 47 duniani, alikuwa akicheza kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Australian Open na ndiye mwanamke Mwingereza pekee aliyesalia katika droo ya mashindano ya mchezaji mmoja mmoja baada ya Heather Watson kushindwa Jumatatu.

Australian Open: Rafael Nadal Aushangaza Ulimwengu
Rekodi: Bibi wa miaka 86 avunja rekodi ya dunia kwa kupanda mlima kilimanjaro hadi kileleni