Watumishi wa afya wametakiwa kuhakikisha wanatakasa kwanza sole za viatu vyao kabla hawajaondoka kwenye vituo vya afya vinavyohudumia wagonjwa wa COVID-19 ili kuilinda jamii na famila zao kwani Sehemu hii ya viatu imebainika kuwa ni nyenzo muhimu ya kubeba virusi vya corona.
Sampuli mbalimbali zilizokusanywa kwenye hospitali ya Huoshenshan inayopatikana Wuhan-China ambacho ndicho kitovu kikuu cha janga hili imebainisha hayo.
Katika kusaidia kusambaa kwa virusi hivyo, Barakoa zote zilizotumiwa na wagonjwa pamoja na watu walio kwenye vituo vyote vya kutibu corona zimetakiwa kutakaswa kwanza kabla hazijatupwa.
Sababu za kufanya hivyo nikuwa, zinabeba majimaji mengi yenye virusi hawa ambao wanaweza kusambaa kwenye vitu vingine hivyo kuongeza kasi ya maambukizi.
Halikadharika watumishi wa afya wanapaswa kutakasa mikono yao mara moja baada tu ya kutoa huduma kwa wagonjwa.