Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), imefanya upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi zaidi ya 15 ikiwa ni awamu ya kwanza katika kuadhimisha miaka 23 tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumzia zoezi hilo Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo Dkt. Laurent Lemeli, amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikifanya upasuaji kwa watoto wasiopungua wanne kila siku.

Mmoja wa wadau waliofanikisha zoezi hilo la upasuaji kwa watoto hao, amewaomba watanzania kujitoa kusaidia matibabu kwa watoto hao ambao wengi wao hutoka katika mazingira magumu.

Kwa upande wake mzazi mmojawapo wa mtoto mwenye tatizo hilo amesema malezi ya mtoto mwenye tatizo hilo yamekuwa changamoto sana kutokana na jamii kuwatenga ikihusisha tatizo hilo na ushirikina.

Taasisi ya MOI inafanya kilele cha MOI Day Septemba 12, kwa kufanya shuguli mbalimbali ikiwemo shughuli za kijamii.

Jaji Mark Bomani kuzikwa Septemba 14
NEMC: halmashauri fanyeni utafiti wa taka