Mshambuliaji nyota wa Napoli SC, Victor Osimhen amefuta picha zote alizokuwa amevaa jezi ya Napoli SC kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Osimhen ambaye ni raia wa Nigeria amefanya hivyo kufuatia vitendo vya ubaguzi wa rangi alivyooneshwa na Napoli SC.

Jana Jumanne (Septemba 26) kupitia ukurasa wake wa Tiktok wa klabu ya Napoli, waliweka video ambayo ilionekana kumdhihaki Osmhen baada ya kukosa penati kwenye mchezo wao dhidi ya Bologna ambao ulimalizika kwa sare tasa.

Video hiyo inamuonesha Osimhen akionesha ishara ya kutaka penati kwa mwamuzi na mwamuzi akatoa, kisha Osimhen akakosa penati hiyo baada ya kuupaisha mpira juu ya lango.

Video hiyo iliwekewa na sauti yenye maudhui ya cartoon. Baada ya muda, Napoli waliifuta video hiyo lakini tayari ilikuwa imewafikia watu wengi. Osimhen anaripotiwa kutopenda kitendo hicho na amepanga kuichukulia hatua ya kisheria klabu yake dhidi ubaguzi huo

Afrika Mashariki wenyeji AFCON 2027
Mitawi ahimiza ulinzi wa Mazingira, Afya ya Binadamu