Rais wa SSC Napoli, Aurelio De Laurentiis ameweka wazi kuwa ifikapo dirisha lijalo la majira ya kiangazi wanaweza kumuuza Mshambuliaji Victor Osimhen ikiwa timu zinazomhitaji zitakubali kuvunja benki ili kumpata.

Osimhen ambaye anawindwa na Arsenal, Chelsea na Liverpool anadaiwa kuuzwa kwa zaidi ya Euro 100 milioni.

Mshambuliaji huyo raia wa Nigeria ameingia kwenye rada ya timu nyingi Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu msimu uliopita ambapo aliisaidia SSC Napoli kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ltalia.

Liverpool ndiyo inadaiwa kuwekeza nguvu zaidi kwenye mpango wa kutaka kumsajili kwa sababu inataka akawe mbadala wa staa kutoka Misri, Mohamed Salah ambaye huenda akatimkia Saudi Arabia mwakani.

Chelsea pia inahangaika kusuka kikosi ambapo upande wa ushambuliaji inatafuta Mshambuliaji atakayeipa mabao zaidi. Mkataba wa sasa wa Osimhen unatarajiwa kumalizika 2025.

Maadhimisho miaka 78 ya UN Oktoba 24
Wachimbaji mkichimba fukieni - Serikali