Mlinda mlango aliyewahi kutamba na mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona Victor Valdes, amezungumza kwa mara ya kwanza tangu alipofanikiwa kuondoka Man Utd.

Mlinda mlango huyo kutoka nchini Hispania kwa sasa ni mchezaji wa klabu ya Middlesbrough, inashiriki ligi kuu ya soka nchini England na tayari ameshacheza mchezo mmoja.

Valdes, amezungumzia mazingira ya soka lake tangu alipotua Old Trafford msimu wa 2014/15 chini ya utawala wa aliyekua meneja klabuni hapo Louis van Gaal ambapo ilifikia hatua walionekana kuwa tofauti.

Valdes amesema maisha ndani ya klabu hiyo hayakua mazuri kama alivyokua anatarajia kutokana na misukosuko ya kuambiwa mtovu wa nidhamu na meneja huyo kutoka nchini Uholanzi, hadi kufikia hatua ya kuambiwa afanye mazoezi na kikosi cha vijana,  japo alitambua ni mapito na ipo siku yangekwisha.

Victor Valdes made his Boro debut against Stoke on SaturdayVictor Valdes akiwa katika mchezo wa kwanza wa ligi ya England msimu huu kati ya Boro na Stoke.

Amesema pamoja na kuamini hivyo, bado alifikiria mambo mengi zaidi, likiwepo suala la kutaka kustaafu soka, lakini alijikaza na kuamini bado safari yake ya soka inaendelea.

Hata hivyo amekiri bado anamuheshimu na ataendelea kumuheshimu Van Gaal kama mzazi wake kutokana na kutambua mchango wake katika maisha yake ya soka tangu alipokua FC Bartcelona.

“Ni vigumu kuelezea, lakini ilikua ni changamoto kwangu, ambayo niliamua kupigana nayo moyoni. Wakati mwingine nilikua sitamani kuendelea kucheza soka kutokana na maisha yale, lakini nilifahamu bado ninahitajika katika jamii ya soka.”

Victor-Valdes-is-a-Boro-manVictor Valdes akiwa katika picha ya pamoja na meneja wa Middlesbrough Aitor Karanka baada ya kusaini mkataba.

“Sina kinyongo na Van Gaal au Manchester United. Alinisaidia wakati wa shida na sasa nina maisha mengine nje ya Old Trafford, daima nitaheshimu mchango alionipa mzee huyu.

“Kwangu ni kama baba mzazi. Sitaki kukumbuka kilichotokea baina yetu zaidi ya kuangalia mbele. Na nikwambie tu, Van Gaal ni rafiki yangu na mara kadhaa tumekua tunazungumza. alisema mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 34 alipohojiwa na Sky Sports News HQ.

TFF Yamruhusu Hassan Kessy Kuitumikia Yanga, Endapo Atalipa Mamilioni
David Moyes Ashtuka, Amrejesha Kundini Lamine Kone