Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kufanya mkutano mkuu wa kidemokrasia kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwenye nyanja za siasa, uchumi na utamaduni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaa, Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa amesema kuwa dhima ya mkutano huo ni  kuhusu ujenzi wa taifa huru la kidemokrasia, hivyo, mada mbalimbali kwenye maeneo ya uhuru, demokrasia na maendeleo zitawasilishwa.

Amesema katika mkutano huo watakuwepo wanasiasa wa vyama mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, wanaharakati mbalimbali, wadau wa maendeleo, watetezi wa haki za binadamu na wananchi
wa kawaida wasio wanachama wa vyama vya siasa, pia taasisi mbalimbali za nje ikiwemo vyama vya Die Linke (Ujerumani), The Altenative (Denmark), PIC Senegal (Senegal), Cyriza (Ugiriki), Labour (Uingereza), na Red Green Alliance (Denmark)

 

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 7, 2017
Video: JPM alivyoiteka Tanga, wananchi walilia kumuona