Chama cha Allience for Democratic Change (ADC) kimelaani kushambuliwa kwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Doyo Hassan Doyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, amesema kuwa matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea nchini hayakubaliki hata kidogo.

Amesema kuwa sehemu zote nyeti zinatakiwa kufungwa kamera ambazo zitakuwa zinarahisisha kwa kiasi kikubwa kufanikiwa kwa upelelezi ambao umekuwa ukichukua muda mrefu.

“Tunaishauri Serikali kuweka kipaumbele katika suala zima la usalama kwani ni kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu yeyote ukiondoa viongozi peke yao, lakini usalama ndio kila kitu,”amesema Doyo

Baba yake Mbwana Samatta aja na kitabu chenye siri ya mwanae
Rich Mavoko aridhia kuvaa fulana ya ‘King Kiba’