Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassima Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.
Majaliwa amesema hayo baada ya mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Katika Mkutano huo ambao Waziri Mkuu amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, amesema nchi za Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na vijijini.
Amesema nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo la kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.
Majaliwa amesema kuwa nchi za Afrika zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia amapendekezo ya kuimarisha uzalishaji wa umeme.
“Tanzania iko vizuri kwa sababu ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme na sasa inamikakati ya kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali.”