Mwanafamilia wa kundi la Navy Kenzo, Aika amemzungumzia mtu aliyeshiriki kuandika shairi lake kwenye ngoma yao mpya ‘Katika’ waliyomshirikisha Diamond.

Tangu ngoma hiyo ilipoachiwa wiki iliyopita na kuwa sehemu ya gumzo mitandaoni, mashabiki wengi waliotoa maoni yao pamoja na wachambuzi wa muziki walikuwa na maoni kuwa sehemu ya Aika itakuwa imeandikwa na Diamond kwani ilikuwa tofauti sana na walichokizoea kutoka kwa mwimbaji huyo.

Hata hivyo, Aika amefunguka kupitia Wasafi TV kuwa mmoja wa watu walioshiriki kwa kiasi kikubwa kuandika sehemu yake ni ‘dansa’ mmoja ambaye ni mwanafamilia wa kundi moja ambalo limeingia katika fainali za shindano la ‘Jibebe Challenge’.

“Hawa [madansa] tuko nao karibu wakati mwingi kwahiyo tunafahamiana. Infact, mtu aliyeshiriki kuandika sehemu ya verse yangu kwenye Katika ni dansa wa kundi moja lililoingia fainali,” alisema Aika.

Mwimbaji huyo ambaye ni mchumba na mama wa mtoto wa Nareel alisema kuwa wanaendelea kuwa karibu na madansa wanaoshiriki shindano hilo na kwamba chochote kinaweza kutokea katika kuboresha muziki wa kundi lao.

‘Katika’ imefanikiwa kwa kiasi kikubwa na huenda ukawa wimbo mkubwa zaidi kwa tarakimu kwa kundi hilo. Tangu ilipoachiwa siku tatu zilizopita, imeshatazamwa zaidi ya mara milioni moja kwenye YouTube na inashika nafasi ya kwanza kwa kuwa gumzo nchini (trending).

Wimbo huo umetumika kuweka wazi kuwa kundi hilo ni sehemu ya familia ya ‘WCB’, wakiwa chini ya meneja Sallam.

Iran yafanya mashambulizi ya makombora kulipa kisasi
Afrika kumpigia kura Gianni Infantino