Wanafunzi wawili wamefariki dunia katika ajali iliyotokea hii leo Jijini Dar es salaam na watu wengine 24 kujeruhiwa huku wengine watatu wakiwa katika hali mbaya.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Superdol barabara ya Nyerere ambapo imehusisha gari aina ya Scania na daladala hivyo kusababisha vifo vya wanafunzi hao.

“Leo imekuwa siku mbaya kwetu kwani ajali hiyo imesababisha vifo vya wanafunzi wawili ambapo watu wengine 24 wamejeruhiwa, dereva wa gari tayari tunamshikilia kwa ajili ya upelelezi,”amesema Sirro.

Hata hivyo, katika hatua nyingine Sirro ameongeza kuwa askali wakiwa katika doria walifanikiwa kukamata risasi ambazo zilikuwa zikitumiwa na waharifu wilaya kigamboni.

Video: CUF waungana na wanahabari kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari
Simba SC Kuipeleka TFF Mahakama Ya Usuluhishi Wa Michezo CAS