Polisi wamezuia kongamano la Bajeti lililokuwa limeandaliwa na chama cha ACT-Wazalendo ambapo kongamano hilo lililenga kumpa fursa kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe kusema yale ambayo angeyasema bungeni baada yeye na wabunge wenzake sita wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bajeti bungeni.

Kufuatia taarifa kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari kwamba kiongozi huyo wa chama alikuwa akitafutwa na polisi bila mafaniko leo June 13 2016 amejitokeza mbele ya wanahabari na kuzungumza.

Mpaka sasa polisi hawajatupa taarifa rasmi kwa nini wamezuia kongamano la bajeti’-Zitto Kabwe

‘Hatufahamu ni nini watawala wanakificha ndani ya bajeti kwani makongamano, mikutano inazuiwa’-Zitto Kabwe

Bofya hapa kutazama alichoongea Mbunge Zitto Kabwe. #Usipitwe

TFF yaanika makundi ya Ligi Daraja la Kwanza
Watanzania wametakiwa kushiriki kupiga vita matukio ya mauaji