Kutokana kuenea kwa taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zikieleza kutiwa mbaroni kwa askofu Kakobe wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGFC) lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametoa ufafanuzi zaidi.

Mambossa amesema kuwa ni kweli walishakuwa katika harakati za kumkamata kutokana na maneno ya kashfa katika mahubiri yake aliyohubiri siku ya ibada ya krismasi.

“Ametoa maneno ya kashfa katika mahubiri yake, lakini sina taarifa kama amekamatwa,” Kamanda Mambosasa alisema na kuongeza” amesema Mambosasa.

“Taarifa za kumkamata zipo, lazima tumkamate. Tutamhoji…tutamhoji alikuwa na maana gani.“Mtu akitenda kosa la jinai ni lazima akamatwe…kwa sasa niko msibani, sijapokea taarifa kama amekamatwa au kuhojiwa. Nitawaarifu kama kutakuwa na taarifa zaidi.” Ameongezea kamanda wa Polisi, Mambosasa.

Meya akunwa na utendaji kazi wa JPM
TFF yakanusha zuio la michuano isiyo rasmi