Binti aliyebakwa katika umri mdogo asimulia namna ambavyo tukio hilo limemuathiri kisaikolojia na kumpelekea kupata maumivu makali yaliyopelekea kufanyiwa upasuaji mara nne bila mafanikio.

Ameeleza kuwa alijaribu kujiua kwa kutumia sumu ambazo alikuwa anachanganya na pombe, lakini pia amewai kutumia sumu ya panya kujiua lakini aliishia kutapika damu hadi pale wasamaria wema walipotokea na kuokoa masiha yake.

Hayo yote amefanya kutokana na kukabiliwa na msongo wa mawazo kufuatia tukio lake la kubakwa akiwa mwenye umri mdogo na alipokuwa na kufahamu namna alivyokuwa akitendewa na kutishiwa ili asiweze kumueleza mtu.

Daktari wa magonjwa ya akili kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Said Kuganda amefafanua zaidi kuhusu ugonjwa wa Sonona ambayo mara nyingi kumpelekea mtu kukata tamaa na kufikiria kujiondoa maisha yake, wapo watu ambao walishindwa kuasidiwa na kufanikiwa kujiua.

Lakini binti huyu mara zote amekuwa akiokolewa na janga hilo la kujichukua maisha yake, tazama hapa katika kipindi cha Afya Tips.

Wadaiwa sugu waundiwa mfumo wa kuwadhibiti
Video: Ukweli juu ya sheria ya Ndoa, Njia za kuoa, umri chini ya miaka 18