Msanii wa maigizo ya uchekeshaji nchini, Pascalia Francis maarufu kama Blackpass ambaye anafanya sanaa hiyo tofauti na ilivyozoeleka huko nyuma amefunguka mtazamo wake juu ya uchekeshaji wa msanii mwenza wa fani hiyo, maarufu kama Ebitoke.

Pascalia ambaye anaigiza kama kiziwi katika vichekesho vyake amesema anachofanya Ebitoke ni kitu cha kawaida sana akidai kuwa tangu akiwa mdogo ameona wachekeshaji wakichekesha kwa namna hiyo mpaka sasa anaona namna hiyo bado inaendelea kutumika hivyo amedai hakuna kitu kipya katika fani ya Ebitoke.

”Anachokifanya Ebitoke naona ni kawaida sana kwangu, nisiwe mnafiki, maana anachokifanya ni kitu ambacho kimefanywa tangu nikiwa mdogo na nimekuwa naona kitu hiko kinafanywa” amesema Pascalia.

Lakini pia ameongezea yupo tayari kufanya kazi na Ebitoke ikitokea utawala wake umemuamuru kufanya nae kazi, ila amedai kuwa hana urafiki na  Ebitoke na hawajawahi kukutana.

Aidha amempongeza kwa kazi anazozifanya na kudai kuwa aongeze bidii kwani anchokifanya ni kitu cha kawaida sana ambacho kilifanywa na kinaendelea kufanywa.

 

Thomas Tuchel kumvua ukocha Arsene Wenger
Nondo aachiwa kwa dhamana