Shehista Alidina maarufu kama Shaykaa ni mfanyabiashara maarufu nchini lakini pia ni muigizaji aliyefanya vizuri katika filamu ya kilio cha baba ambayo kwa inafanya vizuri sokoni.

Kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na magonjwa makubwa matatu  Figo, Endometriosis pamoja na Anemia ugonjwa ambao mtu hupungukiwa damu.

Licha ya kusumbuliwa na magonjwa hayo amekuwa mwanamke mpambanaji na mhamasishaji wa upendo na amani ili kuendelea kutunza familia yake kwani ameolewa na ana watoto wawili.

Msikilize hapa akihadithia namna ambavyo anapambana, japokuwa kuna nyakati alikuwa akikata tamaa lakini anaendelea kumshukuru Mungu kwa kumpigania na kumsimamia vyema katika majukumu yake na katika kutibu maradhi yanayomsumbua.

Tanzania yaichakaza Sudan yatinga fainali CECAFA
Video: Sister Fay afunguka hisia zake kwa Diamond ''mume bora kwangu''