Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna makinda amewataka wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kutanguliza mbele uzalendo kwa kuwajali watoto wa kike ambao wamekuwa wakipata shida kuhusiana na huduma ya vyoo.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuchangia mradi wa ujenzi wa vyoo katika shule mbalimbali za wanafunzi wa kike ambapo amesema jambo hilo ni jema kwa kutoa fursa kwa watoto wa kike kufikia ndoto zao.

Amesema kuwa mtoto wa kike ananafasi kubwa ya kutimiza ndoto zake endapo tu mazingira ya mtoto wa kike atajengewa mazingira rafiki.

“Wabunge mnanafasi ya kuenda mashuleni kuwaelimisha watoto wakike mashuleni ili kuwezo kuwajengea uwezo wa kujiamini,”amesema Ana Makinda

Mnada wa Makontena ya Makonda Wafana Jijini Dar
Video: Majimbo yote 264 ya Tanzania yatajengwa vyoo- Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson