Asasi ya FEDHA imepania kutoa elimu kwa vijana kuhusu uwekezaji na matumizi ya fedha, ili kuweza kuwainua kichumi.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo, Jaffar Seleman alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kuwa lengo la kuanzisha mradi huo ni kutaka kuwakomboa vijana pia kuwaandaa na maisha ya utu uzima kwani vijana wengi wamekuwa hawana tabia ya kujiwekea akiba.
“Sisi tumeamua kutoa elimu kwa vijana ili tuweze kuwakomboa na kuwaandaa katika maisha ya utu uzima, vijana wengi wanapata fedha lakini hawana tabia ya kujiwekea akiba,”amesema Seleman
-
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 11, 2018
-
Tweet ya Kikwete yazua gumzo mtandaoni
-
DC Hapi awafukuza ofisini wabunge wa Chadema