Jeshi la Polisi mjini Kampala, linamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 35, anayejulikana kwa jina la Herbert Kaddu kwa kutaka kujaribu kumpiga panga Askofu Wilberforce Kityo Luwalira wa kanisa katoliki la Mtakatifu Paulo, Namirembe wakati akiendesha ibada siku ya jumapili ya Pasaka.
Kijana huyo, alionekana akiwa ameshika panga na kukimbilia madhabauni alikokuwa padri akiendesha misa, kabla ya kufika madhabahuni kijana huyo alijikwaa katika uzio unaotenganisha madhabau na eneo la waumini.
Hata hivyo alijaribu kuruka kizingiti ili kwenda kwa askofu ambaye wakati huo alikuwa amesimama na msaidizi wake wakiendelea na ibada, na baada ya kuruka alidondoka upande wa madhahabu.
-
Breaking news: Mbowe, viongozi wenzake waachiwa kwa dhamana
-
Magufuli amkubali Goodluck Gozbert kwa ….”Hawawezi kushindana”
Wasaidizi wa askofu huyo walimdhibiti kijana huyo na kumbeba kumwondoa ndani ya kanisa hilo ili asitekeleze kusudio lake.
Taarifa zilizopatikana kanisani hapo zilisema kijana huyo aliwasili kanisani hapo akiendesha gari aina ya ‘kipanya’ Super Custom na kuegesha lango kuu la kuingilia kanisani hapo.
“Alipoingia alimpiga mlinzi wa getini na kuingia kwa nguvu kanisani na alikaa kanisani muda mrefu hadi ibada ilipokaribia kuisha ndipo alipojaribu kwenda madhabahuni,” shuhuda alisema katika video hiyo.
Taarifa ilisema baadaye askari walimkamata na kumpeleka kituo cha polisi Namirembe kwa mahojiano.
Hata hivyo msemaji wa polisi, Patrick Onyango amethibitisha kuwa Kadu alifanyiwa vipimo vya akili na kugundulika kuwa hana tatizo la akili kama ambavyo ilidhaniwa.
Aidha mpaka sasa kijana huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa maelezo zaidi.