Atletico Madrid ikicheza nyumbani katika uwanja wa Wanda Metropolitano, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sevilla katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania La Liga.

Bao la kwanza la Atletico Madrid limefungwa na kiungo Yannick Ferreira Carrasco katika dakika ya 46 kipindi cha pili kabla ya Antonie Griezman kupachika bao la pili dakika ya 69 na kufanya dakika tisini kumalizika kwa Atletico Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sevilla.

Kwa ushidi huo Atletico Madrid inayofundishwa na kocha Diego Simeone imepanda mpaka nafasi ya pili nyuma ya Barcelona ikiwa imevuna jumla ya pointi 14 baada ya kucheza michezo 6.

Tazama magoli ya mchezo huo hapa chini;

Wagonga nyundo wa London washindwa kutamba mbele ya Spurs
Ujauzito wa Kylie Jenner Tyga adai kuhusika