Mwananchi mmoja wa Jijini Arusha amezuiliwa katika hospitali ya Seliani mara baada ya kukosa pesa za kulipia gharama ya matibabu aliyopatiwa.
Dar24 Media imefanya mazungumzo na mkazi huyo wa Jijini Arusha, Joseph Mikaeli Nyangusi na kubainisha kuwa mkazi huyo amezuiliwa katika hospitali ya Seliani iliyopo jijini humo kwa kushindwa kulipa gharama anayodaiwa hospitalini hapo.
Nyangusi amewaomba msaada Watanzania wa kumuwezesha kulipa deni hilo ili aweze kutoka hospitalini hapo ili aweze kuendelea kuihudumia familia yake.
“Tatizo kama hili linaweza kumpata mtu yeyote, hivyo nawaomba Watanzania wanisaidie, na mimi ni binadamu nahitaji kuendelea kuihudumia familia yangu,”amesema Nyangusi
-
Wabunge wazibwa midomo kuhusu Trilioni 1.5
-
Tril 1.5 zataka kumng’oa Waziri, Ndugai amwokoa Mwenyekiti sekeseke la wapinzani bungeni
-
Video: Huu ni ukatili, huwezi kumuua mwenzio kwa wivu wa mapenzi- Dkt. Bisimba