Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limesema kuwa hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa dhidi ya wasanii zina lengo la kuwakumbusha wajibu wao katika kazi wanazozifanya.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Afisa Habari Mkuu wa Baraza hilo, Agnes Kimwaga alipokuwa akizungumza na Da24 Media, ambapo amesema kuwa wasanii wanatakiwa kufuata utaratibu wa kazi zao ili kulinda maadili ya nchi.
“BASATA huwa tunachukua hatua pale tu tunapoona msanii amekiuka maadili, na hili ni kwa nia njema kabisa ya kulinda maadili,”amesema Kimwaga