Beyonce Knowles amerusha kombora kwa mwanamke ambaye anadaiwa kuchepuka na mumewe Jay Z.

Mwanamke huyo wa ‘kizungu’ ambaye anafahamika zaidi kwa wengi kuwa ni mrembo Rachael Roy  alipokea ujumbe mzito kutoka kwa Bey aliyebadili mashairi akiwa kwenye jukwaa la ziara yake na mumewe ya ‘On The Run II’ inayoelekea ukingoni Los Angeles.

Malkia Bey alibadili mistari ya mashairi ya wimbo wa ‘Resentment’ wa mwaka 2006 uliokuwa kwenye albam yake ya ‘B Day’, ili arushe kombora lake.

Mashairi rasmi ya wimbo ni , I’ll always remember feeling like I was no good / Like I couldn’t do it for you like your mistress could.” (Nitakumbuka daima hisia kama vile sikuwa na uzuri wowote/ kama sikuweza kukufanyia kama alivyokuwa anaweza kukufanyia mwanamke wako.

Lakini aliubadili na kumlenga moja kwa moja mwanamke aliyemtaja kama kahaba wa kizungu, ambaye mashabiki wake wengi kupitia mitandao ya kijamii wameeleza kuwa walitambua anayezungumziwa ni ule mchepuko wa Jigga.

“Like I couldn’t do it for you / Like that desperate, mediocre white b*tch could.”

Jay Z alikiri kwenye albam ya 4:44 kuwa aliwahi kuchepuka na kwamba mchepuko huo ulitaka kusambaratisha ndoa yake.

Tetesi za Jay kuchepuka zilifumuka zaidi wakati wa ziara ya ‘On The Run I’ miaka minne iliyopita na kuzua mgogoro ambao ulisababisha mdogo wake Beyonce, Solange kumpiga makofi Jigga kwenye lifti

Hivi sasa wana ndoa hao wanaonekana kuweka mambo sawa wakiwa na watoto watatu, mapacha Rumi na Sir pamoja na dada yao Blue Ivy.

Video: Major Lazer waendeleza mashavu Afrika, ni Mr Eazi na Raye ‘Tied Up’
Uzinzi sasa si kosa la kihalifu