Msanii wa muziki wa Bongo fleva Billnass anayetamba na ngoma ya ‘Tagi Ubavu’ amefunguka kuhusu sababu iliyofanya mistari (Verse) yake kutosikika katika wimbo wa Pochi nene (Remix) wa Rayvanny.
Katika video aliyoipost Rayvanny kwenye mtandao wa Instagram alionekana akiwa na Billnass wakiimba kipande cha mistari aliyoingiza Billnass kwenye wimbo huo kakini wimbo ulipotoka mistari ya Billnass haikuskika.
Billnass amesema wakati wimbo huo unatoka alikuwa na kazi nyingine mkoani na tatizo ni kwamba mwanzo alishiriki katika wimbo wa Rayvanny bila kutoa taarifa kwa usimamizi lakini hana tatizo na Rayvanny.
Tazama video hapa chini Billnass akiongea na Dar24;