Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limetoa maamuzi kuhusu tuhuma zilizokuwa zikiwakabili Wabunge, Freeman Mbowe, Halima Mdee, Ester Bulaya (Chadema) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.
Bunge hilo limefikia hatua hiyo mara baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa na kukiri makosa ambapo waliomba radhi kwa vitendo walivyovifanya.
Aidha, katika taarifa hiyo imesema kuwa wabunge hao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa pamoja wamesamehewa baada ya kukiri makosa yao na kuahidi kutorudia tena.
Hata hivyo, Wabunge wameungana kwa pamoja kuwatetea na kuwaombea msamaha wabunge waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma hizo.