Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini CAG, Profesa Mussa Assad ametetea kauli yake ya kuwa Bunge ni dhaifu na kusema neno hilo amekuwa akilitumia mara kwa mara kwenye ripoti zake.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari saa chache mara baada ya Spika Ndugai kusema ni lazima kiongozi huyo afike kwenye kikao cha kamati ya maadili ili kujibu madai ya kauli yake.

”Mpaka hivi sasa ninaamini nina mahusiano yenye tija kati yangu na Bunge zima na lazima uhusiano huu tuuenzi, na majibu yangu ya kuwa dhaifu ni ya kawaida na hayakuwa na nia ya kudhalilisha Bunge. maneno kama udhaifu, au mapungufu ni lugha za kawaida sana kwa wakaguzi katika maoni ya utendaji na mifumo kwenye taasisi mbalimbali ndiyo maana kwenye ripoti zangu nimelitumia mara kwa mara,”amesema CAG.

Aidha, Kiongozi huyo amesema kuwa Januari 21 atafika mbele ya kamati ya maadili ya Bunge ili kueleza madai yanayomkabili kama barua alivyoipokea januari 15 mwaka huu.

 

 

Tundu Lissu auota urais 2020, atakayeamua siyo Lowassa
Polisi Njombe waeleza matukio ya utekaji na mauaji