Chama cha Mapinduzi CCM kimesema hakitaruhusu chama chake kinajisiwe kwa kuwepo kwa mambo maovu katika uchaguzi mkuu wa Halmashauri Kuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu
Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa uchaguzi huo mpya wa viongozi ndani ya CCM, umedhamiria kujenga CCM mpya itakayofanya kazi kwa ajili ya Watanzania.
“Chama chetu kimejipanga kupata aina ya viongozi ambao ni waaminifu, waadilifu, wachapakazi, wanyeyekevu, wanaweka mbele maslahi ya taifa na chama chetu, ni viongozi wapole lakini wakali sana kwa mambo yasiyo faa, ni viongozi ambao wapo tayari kuwatumikia watanzania, hawa ndio aina ya viongozi ambao wanachama wa CCM wanatuletea ambao watapitia katika uchauzi tunaofanya mwaka huu,” amesema Polepole
Hata hivyo, Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM ameongeza kuwa sasa hivi chama kimejipanga kupata aina ya viongozi ambao ni waadilifu, ili kuijenga CCM imara zaidi, kuweza kuendelea kushikilia dola ya nchi