Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeanza mikakati ya kuhakikisha kinaendelea kushika usukani kwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kuanzia ngazi ya Kata.

Hayo yameelezwa na Makatibu wa Siasa na Uenezi wa hicho wa Kata zote za mkoa wa Dar es Salaam, ambapo wamekutana kwa muda wa siku mbili kwa ajili ya kuanza kupanga mikakati ya kuhakikisha chama chao kinashinda tena kwenye uchaguzi mkuu 2020.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Kata ya Salanga, Mohamed Mjema ambaye amezungumzia mikakati hiyo mbele ya vyombo vya habari kwa niaba ya wenzake,  amesema kuwa wamekaa na kutathmini hali ya kisiasa ilivyo sasa nchini na kuweka maazimio kadhaa ambayo kama yakitumika yatakipa ushindi chama hicho.

Guus Hiddink Aishtukia Leicester City
Kaseja Avunja Ukimya kuhusu Kunyemelewa na Simba na Msimamo Wake